Rais Ebrahim Raisi amesema hayo katika mkutano na waandishi wa habari akiwa pamoja na mwenzake wa Cuba na kusisitizza kwamba, kinachoweza kupunguza vikwazo ni kubadilishana uwezo kati ya nchi hizo mbili.
Rais wa Iran ameongeza kkuwa, nchi hizo mbili zina ushirikiano mzuri katika nyanja za sayansi na teknolojia na moja ya madhihirisho ya hilo ni ushirikiano wa mafanikio baina ya mataifa haya mawili wa kutengeneza chanjo.
Akiashiria kwamba Iran na Cuba zimewekewa vikwazo na Marekani kutokana na kusimama kwake kidete dhidi ya upendaji makuu wa Marekani na kuongeza kuwa, Marekani na mfumo wa kibeberu wanadhani kwamba kwa kuweka vikwazo, wanaweza kuyalazimisha mataifa yaliyoamua kusimama kidete dhidi ya ubeberu yasalimu amri au kukulegeza gamba.Kuhusiana na matukio ya Palestina, Rais Ebrahhim Raisi ameeleza kuwa, wananchi wa Palestina wanaotaka kutetea ardhi yao na maisha yao wameshambuliwa na maadui, na utawala wa Kizayuni kwa moyo wake wa kibaguzi unajihusisha na mauaji ya halaiki na jinai dhidi ya binadamu huko Palestina na kuua wanawake na watoto. Kwa upande wake, Rais wa Cuba Miguel Diaz-Canel amesema katika mkutano na waandishi wa habari na akiwa na mwenyeji wakke Ebrahim Raisi kwamba: "Uhusiano kati ya Tehran na Havana ni wa kihistoria na msingi wake ni heshima na mshikamano, na una historia ya zaidi ya miaka 40.
342/